close menu
Bookswagon-24x7 online bookstore
close menu
My Account
Khamis Abdulla Ameir

Khamis Abdulla AmeirHadithi ya maisha ya Khamis Abdulla Ameir siyo ya kubuni bali ni ya kweli kabisa juu ya mambo yaliyotokea Zanzibar katika kipindi cha kilele cha Vita Baridi, COLD WAR, baina ya nchi za kibepari za Magharibi na zile za kikomunisti za Mashariki. Khamisaliweza kufika London, Uingereza. Huko ndiko alipojitambulisha na kuwa muumini wa siasa za mrengo wa kushoto baada ya kukutana na akina Abdulrahman Mohammed Babu na Ali Sultan Issa na kuhudhuria mikutano na makongamano yaliyokuwa yakiandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha Uingereza na huku akijishughulisha kuwasaidia baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Afrika Mashariki waliokimbilia London kuendelea na harakati zao za kuzikombowa nchi zao ili zipate uhuru. Aliporejea Zanzibar, kabla na baada ya Mapinduzi, Khamis alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi (FPTU). Khamis alikuwa Mjumbe katika Baraza La Mapinduzi (BLM) kwa muda wa miaka minane mfululizo. Alikuwa vile vile Mwenyekiti wa taasisi kadhaa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Kwa hivyo, aliyajuwa mambo mengi yaliyokuwa yakifanywa na SMZ, mazuri na mabaya. Yote ameyaeleza kwa ufasaha mkubwa katika kitabu hiki. Pia, Khamis anaeleza jinsi Hati ya Makubaliano ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ilivyoshindwa kupata ridhaa ya BLM na kusababisha Zanzibar kupoteza uhuru wake kamili wa kujiamulia mambo yake yenyewe. Khamis alikamatwa na kutiwa jela chini ya ukatili wa Mandera (Ba Mkwe), mtesaji maarufu wa watu mahabusi. Aliishi jela kwa muda wa karibu miaka 7 baada ya kuuawa Rais Abeid Amani Karume na yeye kusukumiziwa janga la uhaini. Read More Read Less

2 results found
List viewGrid view
Sort By:
1.
Maisha yangu
No Review Yet
₹2,162
Binding:
Paperback
Release:
11 Mar 2022
Language:
Swahili
Out of Stock
Notify me when this book is in stockNotify Me
2.
Maisha yangu
No Review Yet
₹4,586
Binding:
Paperback
Release:
25 Mar 2022
Language:
Swahili
Out of Stock
Notify me when this book is in stockNotify Me
No more records found
ASK VIDYA